Mzozo wa ardhi Kilifi kupata suluhu

October 11, 2018

Mizozo ya mara kwa mara ya ardhi inayoshuhudiwa kwa sasa katika ardhi ya Kilifi-Jimba kule Watamu kaunti ya kilifi huenda ikapata suluhu hii ni baada ya tume ya kitaifa ya ardhi kuagiza mambwenye wote waliovamia mashamba kufika mbele ya tume hiyo kuhojiwa jinsi walivyopata ardhi hizo.

Kwa mjibu wa kaimu mwenyekiti wa tume hiyo Abigael Mbagaya kuna majina ya maafisaa wa ardhi sawia na mabwenyenye waliotajwa moja kwa moja kwenye kuhusika pakukwa katika uporaji wa ardhi za wenyeji katika eneo hilo.

Kulingana na Mbagaya amehoji kuwa tume hiyo iko tayari kusikiliza maoni kwa siku ya tatu kutoka pande zote mbili ikiwemo maskwota na wamililiki halali wa ardhi hizo zenye utata.

Aidha Mbagaya amesisitiza kuwa serikali kupitia tume hiyo haitarusu visa vya wakazi ama mabwenyenye kuvamia ardhi ambazo sizao  na kwamba shoka la kuwafurusha litawapata.

Taarifa na Charo Banda.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.