Naivas yafungua duka jipya Likoni

December 4, 2018

Kufunguliwa kwa duka jipya la Naivas katika eneo la Likoni Kaunti ya Mombasa kutapanua zaidi shughuli za kibiashara miongoni mwa wawekezaji na Wafanyibiashara wadogo wadogo wa Pwani.

Afisa mkuu anayesimamia maswala ya kibiashara katika maduka ya Naivas nchini, Willy Kimani, amesema duka hilo limeangazia mno ushirikiano wa kibiashara na Wafanyibiashara wadogo wadogo na makampuni makubwa ili kuipanua Kaunti hiyo kibiashara.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa duka hilo lililo katika eneo la Nakumatt ya zamani huko Likoni Kaunti ya Mombasa, Kimani hata hivyo amezitaka Serikali za Kaunti hapa Pwani kupunguza gharama za kufanya biashara ili kuona kwamba wawekezaji zaidi wanaliangazia eneo la Pwani ili kuliinua kiuchumi.

Kimani amewarai wakaazi wa eneo la Pwani kuzuru maduka ya Supermarket ya Naivas katika maeneo ya Ukunda, Likoni, Kenol kwenye barabara ya kutoka Mombasa kuelekea Malindi ili kupata bidhaa  aina mbalimbali.

Usimamizi wa maduka hayo ya Naivas nchini unapania kufungua duka la 49 katika eneo la Mwembe tayari juma lijalo.

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.