Napenda sana kununua pamba – Totti

November 25, 2017

Mtayarishaji wa mziki kutoka ukanda wapwani maarufu kwa kama Totti amefunguka na kueleza kitu anakipendelea kukifanya na pesa anazopata.

Akizungumza na Uhondo Totti amesema kuwa ana upungufu wa kupenda kununua mavazi na sana sana yeye hupendelea kununua viatu.

“Napenda sana kununua mavazi na inapokuja kwa viatu mimi huvinunua mara kwa mara. Wiki haiwezi pita kabla sijafanya shopping ya viatu,” amesema Totti.

Kulingana na Totti muonekano kwa msanii ni muhimu sana na ndio maana yeye hupendelea kununua mavazi mapya ili aonekane nadhifu.

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.