NCCK YATAKA UFISADI UTANGAZWE JANGA LA KITAIFA

June 6, 2018

Baraza la makanisa nchini ukanda ya pwani linamtaka raisi Uhuru Kenyatta kutangaza ufisadi kama janga la kitaifa.

Mwenyekiti wa baraza hilo pwani kasisi Lawrence Dena amesema ufisadi ndio chanzo cha masaibu yanayomkumba mwananchi ikiwemo umasikini.

Kasisi Dena ametoa wito kwa serikali kufanya uchunguzi wa kina na kuwatambua maafisa wanaoendeleza ufisadi na kuwafungulia mashtaka ili mali ya umma irudishwe.

Aidha amependekeza kubadilishwa kwa hukumu ya ufisadi kuwa kifungo cha maisha kwa wale watakaopatikana na hatia kwenye sakata za ufisadi.

Taarifa na Marietta Anzazi

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.