Nikimpata Hamisa nitamuumiza tu – Otile Brown

June 25, 2018

OTILE BROWN

Msanii Otile Brown amejipiga kifua kwa kukiri kuwa iwapo atatoka kimapenzi na Hamisa Mobeto basi atakuwa anamuumiza tu kwani amaezoe vitu vikubwa.


Otile alikuwa akizungumza na kituo kimoja cha runinga nchini Tanzania alipotoa kauli hiyo.

“Nimezoea vikubwa nikipata vidogo nitakuwa naviumiza tu,” amesema Otile Brown.

Aidha msanii huyo ameelezea kupendezwa na warembo wa kutoka Tanzania na kukiri kuwa kidogo ateleze mtegoni.

Otile anatoka kimapenzi na mwilimbwede Verah Sidika. Kwa sasa yupo nchini Tanzania anakoendeleza kusukuma kazi zake.

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.