NTSA yaombwa kusirikiana na shule za udereva

March 14, 2019

Mamlaka ya kudhibiti  uchukuzi na usalama  nchini NTSA imeombwa kushirikiana vyema  na shule za udereva katika kuhamasisha madereva kuhusiana na  Rasimu  ya  masomo mapya ya udereva kabila ya mfumo huo kuanzishwa kutekelezwa rasmi.

Kulingana na  mwenyekiti wa shule za udereva ukanda wa Pwani  John Magara amesema kwamba idadi kubwa ya maderava  nchini  hawanaufahamu kuhusiana  na masomo mapya huku akisema  tayari sheria za  Rasimu hiyo zilikuwa zinatumika bararbarai hatua aliyoitaja kupelekea changamato kwa madereva.

Akiongea kwenye warsha iliyowaleta  pamoja wadau wa NTSA na wamiliki wa shule za udereva ukanda wa pwani magara amesema kama viongozi hawataruhusu kamwe rasimu hiyo kutumika kama sheria mpaka pale mamlaka hiyo itakapopata maoni mwafaka  kutoka kwa wadau wa sekta hiyo.

Kwa upande wake  Naibu mkurugenzi kwenye kitengo cha usalama wa barabarani ndani ya mamlaka hiyo  Duncan Kibogong  Cheriyot NTSA imekanusha madai kwamba Rasimu ya masomo mapya ya udereva haujulikani kwani amesema tayari wameanzisha zoezi la kukusanya maoni kutoka kwa wadau wa shule za uderava nchini.

Taarifa na Hussein Mdune.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.