NYOTA WA PWANI WAKABANA KOO

April 15, 2018

Timu ya kandanda ya Taita Taveta All Stars imeendelea na ushupavu wake wa kutopoteza mechi yoyote baada ya kuandikisha sare ya mabao 2-2 na Kilifi All Stars.

Kwenye mechi iliyosakatwa uwanjani Dawson Mwanyumba mapema hii leo, Kilifi All Stars walitangulia kutingisha nyavu kabla ya Alik Aziz kurejesha bao hilo dakika moja baadae. Charles Onyango aliongeza bao la pili kwa vijana wa nyumbani kabla ya Kilifi All Stars kuwanyamazisha mashabiki wa nyumbani dakika nne kabla ya refa kutamatisha mchuano.

Kwa sasa Taita Taveta All Stars wanashikilia nambari mbili kwa alama saba (7).

Taarifa na Fatuma Rashid.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.