Ombi la Timamy latupiliwa mbali na Mahakama

May 17, 2018

Mahakama ya Rufaa huko Mombasa imetupilia mbali ombi la aliyekuwa Gavana wa Lamu Issa Timamy la kutaka kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi dhidi ya gavana wa sasa Fahim Twaha kusikilizwa katika Mahakama ya Rufaa jijini Nairobi.

Akitoa uamuzi huo, Jaji wa Mahakama hiyo Wanjiru Karanja amesema ombi hilo limekatiliwa kutokana na malalamishi yaliotolewa na mawakili wa Issa Timamy kutokuwa na msingi wowote.

Jaji Karanja ameeleza kuwa hata kesi hiyo ingepelekwa jijini Nairobi bado isingebadilisha uamuzi wa Mahakama wa kuitupilia mbali kesi hiyo.

Timmamy aliyekuwa gavana wa Lamu aliwasilisha kesi hiyo mahakamani akipinga kuchaguliwa kwa gavana wa sasa Fahim Twaha kwa madai kuwa Twaha hakushinda uchaguzi huo kwa njia ya huru na haki.

Taarifa na Radio Kaya.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.