Ombi la wahanga wa mafuriko la kupewa kondomu latimizwa

May 3, 2018

Ombi la wahanga wa mafuriko kaunti ya Kilifi la kupewa mipira ya kondomu limetimizwa.

Wahanga hao walikuwa wameviomba vyombo vya serikali kutumiwa mipira hiyo ili kuepukana na kuambukizwa kwa maradhi ya zinaa.

Wahanga hao walikuwa wamehoji kuwa kukusanyika kwao mahali pamoja kulikuwa kumeongeza kasi ya vishawishi vya kushiriki mapenzi hivyo basi kuitisha kinga hiyo.

Akizungumza kuhusiana na swala hilo waziri  wa Afya wa kaunti hiyo Anisa Omar amewashukuru wahanga hao kwa kujitokeza kimasomaso na kuitisha kinga akisema kuwa ni hatua moja wapo ya kupunguza maambukizi.

Aidha ameongezea kuwa ni haki ya kikatiba kwa kila mwananchi kupewa vifaa vya kulinda Afya.

Taaarifa na Radio Kaya.

 

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.