Oparesheni peleka mtoto shule yaendelezwa Malindi

February 8, 2019

Maafisa wa utawala eneo la Malindi kaunti ya Kilifi, sasa wanaendeleza mabaraza mbalimbali katika kila shule za msingi ili kuhakikisha watoto wanazingatia masuala ya elimu.

Naibu Chifu wa kata ndogo ya Shela kule Malindi Nicodemus Mwayele, amesema lengo la mabaraza hayo ni kuhakikisha watoto hawasalii nyumbani bali wanaenda shuleni.

Mwayele amewaonya wazazi watakaosalia na watoto wao nyumbani kuwa watakabiliwa na mkono wa sheria.

Aidha amehoji kuwa watafanya msako mkali hivi karibuni kwenye vijiji vyote vya eneo hilo la Shela ili kuhakikisha agizo la serikali la watoto kwenda shule linatekelezwa.

Taarifa na Charo Banda.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.