PAT C arudia uimbaji

May 14, 2018

Msanii PAT C amerudi tena kwenye ulingo wa uimbaji baada ya kimya kirefu.

Msanii huyo amerudi na kibao kinachofahamika kwa jina “Naunewe”. Utunzi huu ameufanya kwa ushirikiano na msanii Sha Biggy.

Awali msanii huyo alikuwa ameambia Uhondo kuwa ameachana na mziki kwani haukuwa na faida kwake.

Uhondo imebaini kuwa amerudi katika ulingo wa sanaa baada ya kupata ufadhili kutoka kwa mwana biashara mmoja kutoka Kilifi.

Miaka ya nyuma Pat C aliwik ana kibao “Nakuhenza Mche”.

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.