Phat S azungumzia uvumi wa kifo chake

May 25, 2018

Ni hali ya kushtua kusikia au kusoma tangazo la kifo chako, Je utafanya nini iwapo utapata kuona jumbe za rambi rambi za kifo chako unapofungua simu yako?

Hali hii ilimkumba msanii Phat S hivi majuzi.

Akizungumza na Uhondo kuhusu tukio hilo Phat S aliyekuwa na unyonge mwingi kwenye sauti yake amekiri kuwa amepitia kipindi kigumu sana baada ya watu wasiojulikana kutangaza kifo chake katika mitandao ya kijamii.

“Ni jambo lilonishtua na sijui aliyefanya hivyo ana madhumuni gani, nimeshindwa kufanya chochote nimebaki kuumwa na kichwa,” amesema Phat S.

Aidha amefichua kuwa tayai amepiga ripoti kwa maofisaa wa polisi ili wafanye uchunguzi.

“Nilienda polisi kupiga ripoti na kujaribu kufuatilia na kampuni moja ya mawasiliano lakini bado sijamjua aliyeanzisha uvumi huo ni watu wengi waliandika ujumbe wa kifo changu,” amesema Phat S.

Msanii huyo amewaomba watumizi wa mitandao ya kijamii kuwa makini wanapotumia mitandao hiyo.

“Jamani kama mumekosa la kufanya kwenye mitandao ya kijamii, tafuteni la kufanya lakini sio kuuwa wenzenu,”amesema Phat S.

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.