Picha za uhusiano kati ya Avril na VBO Micharazo zaibuka

November 27, 2018

Wanasema penzi ni kama nyasi likiota halifichiki na linaweza kuota popote pale. Kama nyasi zinavyoweza kuwa magugu penzi pia husalia kuwa historia wakati mwingine.

Katika kisa cha hivi majuzi picha za zamani za muimbaji Avril na VBO Micharazo zimeibuka mtandaoni.

Wengi wetu tunamfahamu Avril ila kwa wale wasiomujua VBO Micharazo huyu ni msanii aliyetesa enzi zake na vibao kama vile “Kamoja tu” na “Nasikia utamu tam” akiwa chini ya kundi la Bugz pamoja na msanii Bobby Mapesa.

Kwenye picha hizo zinazoaminika kuwa zilipigwa katika hoteli moja mjini Watamu Avril na Micharazo wanaonekana wakiwa na wakati mzuri.

Taarifa na Dominick Mwambui.

 

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.