POLISI WACHUNGUZA SHEHENA YA SUKARI – KIJIPWA

June 14, 2018

Polisi kaunti ya Kilifi wananedelea na uchunguzi kuhusiana na lori tatu zilizokuwa zimebeba tani 86 za sukari gushi zilizokamatwa mwishoni mwa juma katika kizuizi cha trafiki eneo la Kijipwa.

Kamanda wa polisi wa kaunti ya Kilifi Fedrick Ochieng amesema sukari hiyo kutoka nchini Brazil ilikuwa ikisafirishwa hadi kaunti ya Garisa.

Ochieng amesema kwamba kulingana na sikabadhi zilizopatikana ni kuwa sukari hiyo ilikuwa inasambazwa kwa kampuni ya MACKEN ZIE EA LTD na ilitengenezwa mwezi Juni 2017 na itaharibika 2020.

Aidha  maafisa wa mamlaka ya mapato nchini (KRA) na wale wa mamlaka ya kuthathimini ubora wa bidhaa nchini KEBS wameweza kufika katika kituo cha poilisi cha Kijipwa ambako sukari hiyo inazuiliwa na kuthibitisha kuwa sukari hiyo ni gushi huku wakichukua sampuli kwa uchunguzi zaidi.

Taarifa na Marieta Anzazi.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.