“Polisi wanaodhulumu wananchi chuma chao kimotoni,” asema Ipara

May 14, 2018

Idara ya usalama kaunti ya Mombasa imeahidi kuwakabili kisheria maafisa wa polisi wenye tabia ya kuwadhulumu wananchi.

Akiongea katika warsha ya kuvizawadi vitengo vya usalama katika eneo la Likoni na Changamwe kutoka kwa shirika la kupambana na madawa ya kulevya na ufisadi la UNODC kamanda  mkuu wa polisi kaunti ya Mombasa Johnstone Ipara amesema kuwa afisa yeyote wa polisi atakayepatikana na makosa atakabiliwa kisheria.

Ipara ametaja kuwa maafisa wa polisi wana jukumu la kushirikiana vyema na wananchi kuukabili uhalifu ili kuhakikisha visa vya uhalifu vinapungua Mombasa.

Kamanda huyo wa polisi amewataka wazazi Mombasa kuwa karibu na vijana ili kuwasaidia kujitenga na utumizi wa mihadarati.

Taarifa na Hussein Mdune.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.