Produza Baindo amtaliki mkewe

January 8, 2019

BAINDO

Mtayarishaji wa mziki maarufu ukanda wa Pwani Produza Baindo amemtaliki mke wake.

Baindo alikuwa katika ndoa na msanii Shinny Ann na wameajaliwa mtoto mmoja.

Sababu kuu iliyopelekea wawili hao kuachana haijabainika ila Baindo haonekana kuangalia nyuma tena.

Kupitia kwa ukurasa wake wa Facebook amewafahamisha mashabiki kuwa wawili hao sio mke na mume na watu waache kumhusisha na Ann ambaye amemzalia mtoto mmoja.

Taarifa na Dominick Mwambui.

 

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.