Radio Kaya FC waandikisha sare katika mechi ya ufunguzi

June 16, 2018

Radio Kaya FC imetoka sare butu na kikosi cha soka cha NTV katika mashindano ya soka  wachezaji watano kila upande yanayoendelea katika uwanja wa Mkomani kaunti ya Mombasa.

Mashindano hayo ambayo yamedhaminiwa na kampuni ya mawasiliano nchini Safaricom yanajumuisha vyombo vya habari kutoka ukanda wa Pwani.

Kikosi cha Radio Kaya Fc kinachoongozwa na nahodha Teddy Tinga kimepangwa kwenye kundi moja na Safaricom FC (wamejiondoa), NTV, KBC na Gazeti la The Coast.

Wachezaji tajika katika kikosi hicho ni mtangazaji wa Kaya Flavaz Sista Shaniz, msomaji habari na mtangazaji msaidizi wa kipindi cha Misakato ya Bango Mwahoka Mtsumi, Hassan Yawa, waandishi Michael Otieno,Hussein Mdune, Cyrus Ngonyo,Salim Mwakazi,  mchekeshaji Kura Tsuma maarufu kama Kalambua, na mtangazaji wa kipindi cha Mirindimo Ya Kimwambao Fatuma Mwangala maarufu kama Toto Bomba.

Mshindi wa kwanza katika mashindano hayo ataondoka na kitita cha Ksh 50,000. Mshindi wa pili ataondoka na Ksh 30,000 na mshindi wa tatu atajinyakulia Ksh 20,000.

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.