Radio Kaya FC yawania Ksh 50,000 katika shindano la Safaricom

June 16, 2018

Kikosi cha Radio Kaya cha wachezaji wa soka kinazidi kuwania shilling elfu hamsini kwenye shindano la wachezaji watano kila upande la soka linaloendelea katika uwanja wa Mkomani mjini Mombasa.

Kikosi hicho kikiongozwa na Nahodha Teddy Tinga kimeratibiwa kukutana na Safaricom FC, NTV, KBC na Gazeti la The Coast.

Wachezaji tajika katika kikosi hicho ni Sista Shaniz, Hussein Mdune, Cyrus Ngonyo, Mwahoka Mtsumi, Hassan Yawa, Michael Otieno, Kura Tsuma maarufu kama Kalambua, Fatuma Mwangala maarufu kama Toto Bomba na Salim Mwakazi.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.