Radio Kaya kutumia michezo kupambana na Mihadarati

April 13, 2018

Kituo nambari moja ukanda wa Pwani Radio Kaya kikishirikiana na wadau wengine wameanza kampeni ya kupambana na utumizi wa mihadarati katika jamii.

Kwenye kampeni hiyo iliyo na kauli mbiu ” Kataa Mihadarati Kataa Uhalifu” kupitia kwa mradi wa Samba Sports Youth Agenda mchezo wa mpira wa miguu utatumiwa kuwaelimisha watoto wadogo kuhusu athari za mihadarati na maadili machafu.

Kulingana na mshirikishi wa Samba Sports Youth Agenda Mohamed Mwachausa mradi huo unalenga kuwaepusha vijana kutoka kaunti ya Kwale dhidi ya Itikadi kali ikizingatiwa kuwa eneo hilo limepoteza zaidi ya vijana 35 kwa mtutu wa bunduki. Vijana hao walikuwa washukiwa wakuu wa mashambulizi ya kigaidi.

Vilevile ameongeza kuwa idadi ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI yapo juu katika kaunti hiyo hivyo basi ni sharti juhudi ziwekwe katika kuwalinda vijana.

Taarifa na Dominick Mwambui.

 

 

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.