Raila Odinga aunga mkono ukaguzi wa mali za maofisaa wa serikali

June 18, 2018

Kinara wa mrengo wa upinzani nchini CORD Raila Odinga akiwahutubia Wakaazi katika eneo la Msambweni Kaunti ya Kwale. Raila ameikosoa Serikali ya Jubilee kwa kushindwa kulitatua tatizo la ardhi katika Ukanda wa Pwani.

Picha/Maktaba

Mombasa , KENYA – Kinara wa Chama cha Odm Raila Odinga, sasa ameunga mkono agizo la rais Uhuru Kenyatta la kufanyiwa ukaguzi wa maafisa wote wa serikali ili kubaini jinsi walivyopata mali wanayomiliki huku akisema yuko tayari kukaguliwa.

Akizungumza mjini Mombasa wakati wa Kongamano la chama hicho, Raila amesema hatua hiyo itasaidia kutambua jinsi kila mmoja alivyopata mali anazomiliki, akisema baadhi yao wamepora raslimali za umma na kujinufaisha binafsi.

Raila amehoji kuwa anaunga mkono kikamilifu vita dhidi ya ufisadi humu nchini, akisema jinsi hali ilivyo kwa sasa ni wazi kuwa taifa haliwezi kupiga hatua zozote za kimaendeleo iwapo janga hilo halitakomeshwa.

Aidha amewahakikishia wananchama wa Odm kuwa maridhiano kati yake na rais Kenyatta ni kwa manufaa ya wananchi ili kuliwezesha taifa hili kusonga mbele na kuimarika kiuchumi.

 

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.