Rais Kenyatta ashauriwa kulitilia manani swala la Pwani kujitenga

December 1, 2017

Mashirika ya kijamii hapa Pwani yanamtaka Rais Uhuru Kenyatta kutolipuza swala la Pwani kujitenga na sehemu ya bara ya Kenya.

Mashirika hayo yakiongozwa na Shirika la KECOSCE chini ya Mkurugenzi wake mkuu, Phyllis Muema yamesema kuwa swala la kujitenga sio swala dogo na kutokana na kauli ya Rais Kenyatta kuwa atawaunganisha wakenya wote basi hana budi ila kulitathmini swala hilo.

Akizungumza mjini Mombasa, Phyllis amesema kuwa ni sharti mikakati mwafaka kuidhinishwa ili taifa liungane hasa baada ya mgawanyiko mkubwa wa kisasa na kikabila kushuhudiwa humu nchini.

Wakati uo huo, amemtaka Rais Kenyatta kufanya mkutano na mashirika yasiokuwa ya kiserikali ili kujadili jinsi Serikali itakavyofanya kazi na Mashirika hayo sawia na kuwaunganisha wakenya.

Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.