Ray  C amsumbua Chipukizi kuwaasia vijana baada ya kutumia mihadarati kwa miaka 9

June 26, 2018

Ray C ameweka wazi kuwa aliweza kulimwa na jinamizi la mihadahariti kwa miaka 9 kabla ya kujinasua.

Akiongea mjini Mombasa Ray C ameseweka kuwa mihadhari iliweza kumulemaza kimwili na hata kwenye   talanta yake ya mziki.

Ray C ambaye aliweza kuvuma na kibao cha “wanifuatia nini” ameyataja madawa ya kulevya kama adui mkubwa wa wanadamu hivyo basi akawataka vijana kujiepusha na utumizi wa mihadaharati.

“Kuna haja ya jamii kwenye mataifa ya kiafrika kuwajali watu walioathirika na madawa yakulevya na kama umeathirika na madawa ya kulevya usione aibu kujitokeza,”amehoji Ray C.

Msanii huyo ameweka wazi kuwa amekuwa akimsumbua mkurugenzi mmoja wapo wa NACADA, mchekesahji Chipukizi ampe nafasi ya kuzungumza na vijana.

“Niliweza kumsumbua Chipukizi kwa Facebook, Instagram na kumwambia kuwa niko Nairobi na ningetaka kufika Mombasa kujiunga na vijana kuwaelimisha kuhusu madhara ya madawa ya kulevya”, amesema Ray C.

Msanii huyo nguli amesema kuwa tangu atoke kwenye kituo cha kurekebisha tabia nchini Tanzania ametimiza miaka mitatu sasa. Hatua anayoitaja kumurudishia amani yake ya Maisha ya zamani.

Taarifa na Hussein Mdune.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.