Reachout kuungana na NACADA

February 10, 2019

Shirika la kupambana na mihadarati na vileo haramu nchini NACADA litashirikiana na lile la kupambana na uraibu wa dawa za kulevya Pwani katika mikakati ya kuwarekebisha watumizi wa dawa za kulevya katika eneo hili.

Mkurugenzi wa Shirika hilo Kanda ya Pwani George Karisa amesema kwamba ushirikiano huo unatokana na changamoto ya vijana wadogo kujitosa katika uraibu wa dawa za kulevya bila ya kuwepo na mipangilio mwafaka ya kuwanasua.

Akizungumza baada ya kutia sahihi mkataba huo wa miezi mitatu Karisa amesema kwamba waraibu wa dawa za kulevya watanufaika na matibabu na ushauri katika kituo cha kuwarekebisha waraibu cha Reachout Centre Trust kilicho katika ‘Kona ya Mtongwe’ huko Likoni.

Karisa amesema kwamba baada ya miezi hiyo mitatu Mashirika hayo mawili yatakadiria matokeo ya mradi huo kabla ya kuidhinisha mipangilio mingine ya kuuendeleza mpango huo unaolenga kupiga jeki vita dhidi ya utumizi wa dawa za kulevya miongoni mwa Vijana hapa Pwani.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.