Ruto asisitiza kuwa marufuku ya sandarusi itaendelea nchini

June 5, 2018

Naibu rais William Ruto amesema serikali haitalegeza kamba katika marufu ya utumizi wa mifuko ya plastiki ilioanza kutekelezwa mwaka uliopita.

Akihutubu kwenye maadhimisho ya kitaifa ya siku ya Mazingira ulimwenguni, yalioandaliwa mjini Kwale, Ruto amedokeza kuwa zaidi ya tani milioni 2 za plastiki huingizwa humu nchini kila mwaka, jambo anasema kama tishio kuu la Mazingira.

Naibu rais amehimiza watengenezaji bidhia humu nchini kubuni mifuko mbadala itakayotumika na wananchi mbali na mifuko ya plastiki.

Kando na hayo Ruto, ameahidi kuwa serikali kuu pamoja na zile za kaunti hasa ukanda wa Pwani zitashirikiana ili kuimarisha upanzi wa miti ya mikoko, akisema miti hiyo ni ya manufaa kwa mazingira.

Kwa upande wake Gavana wa Kwale Salim Mvurya ameipongeza serikali kuu kwa kuandaa maadhimidho hayo katika kaunti ya Kwale, akisema hatua hiyo imeafikiwa kutokana na sifa za Kwale kwenye masaula ya usafi wa mazingira.

Taarifa na Michael Otieno.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.