Sababu kwa nini mwili wako huwasha baada ya kuoga

February 10, 2019

Picha kwa hisani.

Je unajua kwa nini wewe huwashwa baada ya kuoga? Kama jibu lako ni la usitie shaka leo utafahamu sababu kwa nini hali hii hukupata.

Hali ya kuhisi kuwashwa katika sehemu mbalimbali za mwili baada ya kuoga ni hali inayowapata wengi ila sio wote wanaofahamu chanzo chake.

Kulingana na wataalam wa ngozi sababu zifuatazo ndizo husababishwa mwasho baada ya kuoga.

Ukavu wa mwili au Xerosis hupata watu wa kila umri lakini huwa sana miongoni mwa wazee.
Hali hii hujitokeza pale ngozi yako inapokosa unyevu. Hii ni baada ya kuoga na maji moto au kutumia sabuni ambazo hukausha ngozi.

Ukavu wa ngozi pia unaweza kutokana na ukosefu wa vitamini A na B mwilini.

Sabuni unayotumia pia inaweza kuwa inachangia mwasho iwapo kemikali zilizotumiwa ni kali kwa ngozi yako.

Ili kukabiliana na hali hii wataalam wa ngozi wanashauri kuwa utumie loshoni itakayoweka unyevu kwenye ngozi yako muda mfupi tu baada ya kuoga. Usijifute na taulo bali jipake loshoni ukiwa bado upo na majimaji mwilini.

Vile vile unaweza kujaribu sabuni tofauti tofauti ili ubaini ni sabuni gani ambayo sio kali kwa mwili wako.

Ulaji wa mboga na matunda kwa wingi pia kutakusaidia kupata vitamini muhimu mwilini zitakazokusaidia kukabiliana na hali hii.

Taarifa na Dominick Mwambui.

 

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.