Sababu ya Susumila kukataa kolabo ya Otile yafichuka

January 22, 2019

SUSUMILA

Msanii Yusuf Kombo maarufu kama Susumila amefunguka na kueleza sababu zilizomfanya kukataa kolabo na msanii Otile Brown.

Kulingana na msanii huyo anayetamba na kibao Unanimaliza alichomshirikisha Jolie kutoka Tanzania ni kuwa Otile alimnyima uhuru wa utunzi.

Susumila anadai kwamba Otile aliandika nyimbo na hakumtaka Susumila kubadilisha wala kuongeza chochote katika wimbo ambao walikuwa wanafaa kufanya pamoja.

Kutokana na hilo Susumila ameamua kushika zake hamsini huku Otile naye akielekea njia tofauti.

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.