Sahau Camp Mulla kutana na Dice Gang

November 30, 2017

Tasnia ya burudani nchini imepata kipenzi kipya katika mziki wa aina ya Hip Hop na RnB.

Baada ya kuyumba kwa kundi la Camp Mulla sasa kundi la Dice Gang limeijaza nafasi hiyo.

Kundi hilo lililo chini ya meneja Nasib Sulubu limeitweka mioyo ya wengi licha ya kuwa katika ulingo wa burudani kwa miaka miwili pekee.

“Haijakuwa rahisi lakini tunashukuru mapokezi tuliyopata. Lengo letu ni kufikia soko la kimatifa,” amesema meneja huyo.

Kundi hilo linalojumuisha msanii Rapkeed, Aruchii na Tyno limekuwa kipenzi cha wengi na kibao chao kipya kwa jina Am In Love.

Taarifa na Dominick Mwambui.

 

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.