Samba sports kuwahusisha walemavu

June 26, 2018

Shirika la Samba Sports linalohusika na kuwahamasisha vijana kuhusiana na madhara ya utumizi wa mihadarati na uhalifu kupitia michezo kaunti ya Kwale, limeweka mikakati ya kuihusisha jamii ya watu wenye mahitaji maalum katika mpango huo.

Akiongea na mwanahabari wetu Mshirikishi wa shirika la Samba Sports Mohammed Mwachausa amesema kuwa amejadiliana na viongozi wa vijana wanaoishi na ulemavu  na mipangilio ya kuwahusisha itafanyika karibuni.

Mwachausa  ametaja kuwa vijana hao watahusishwa pia kwani wao pia huathirika na utumizi wa mihadarati na uhalifu ambao huathiri talanta zao.

Mshirikishi huyo ameihimiza jamii kuendelea kushirikiana kwa karibu na shirika la Samba Sports ili kuhakikisha suala na mihadarati linazikwa kwenye kaburi la sahau ili kuwawezesha vijana kukuza vipaji vyao.

Taarifa Mariam Gao.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.