‘Sauti 47’ yaisaidia serikali kutatua shida za vijana

July 21, 2017

Mwenyekiti wa shirika la kupambana na mihadarati na vileo nchini (NACADA) Luteni Kanali Julius Githire amesema mradi wa ‘Sauti 47’ utaisaidia serikali kutatua matatizo ya vijana.

Kulingana na mwenyekiti huyo, mradi huo uliozinduliwa na Wizara ya maswala ya ndani kwa ushirikiano na afisi ya Rais na shirika la NACADA unalenga kukutana na vijana katika kaunti zote 47 nchini.

Githire aliyekuwa akiwahutubia zaidi ya vijana elfu moja katika ukumbi wa Chandaria kwenye chuo cha mafunzo anuwai cha MTTI huko mjini Mombasa amesema ni lazima vijana wenyewe wachukue jukumu na kujitenga na utumizi wa mihadarati.

Mwenyekiti huyo hata hivyo amesema kuwa Shirika hilo litajitahidi  kuwatibu watumizi wa dawa za kulevya na kuidhinisha vituo zaidi vya kuwarekebisha watumizi hao.

Taarifa hii imeandikwa na Gabriel Mwaganjoni.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.