Sekta ya utalii yatarajiwa kuimarika

December 1, 2017

Meneja wa hoteli moja mjini Malindi Paul Sawe amesema kuwa wanatarajia sekta ya utalii hapa Pwani kuimarika zaidi baada ya hafla ya kuapishwa kwa Rais Uhuru Kenyetta.

Sawe amesema  biashara iko chini tangu mwaka wa 2013 na ikaongezeka tu mwishoni mwa mwaka 2015 huku akisema kuwa usalama duni wa watalii wanaozuru maeneo ya Pwani ndio chanzo cha kudorora kwa sekta hiyo.

Sawe ameitaka serikali kuu kuhakikikisha inaifufua sekta ya utalii ili kuinua maisha ya wakaazi wa Pwani.

Kauli yake imeungwa mkono na mfanyibiashara Nickson Mramba ambaye pia ni Mwakilishi wa wadi ya Kakuyuni kaunti ya Kilifi ambapo amehoji kuwa Rais Kenyatta ana jukumu la kuhakikisha sekta ya utalii inarudi katika hali yake ya kawaida.

Taarifa na Charo Banda.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.