Seneta awahimiza wasanii kugeukia miradi mbadala

May 28, 2018

Seneta mteule Christine Zawadi amewahimiza wasanii ukanda wa Pwani kugeukia miradi mbadala ya kiuchumi ili waweze kujikimu kimaisha.

Akizungumza na Uhondo alipokuwa anahudhuria mazishi ya msanii Bob Mwayele huko Gongoni, Zawadi amesema kuwa wasanii wengi huishia kufa maskini kwa sababu hawana miradi mbadala ya kuwasaidia kujikimu kimaisha.

Kulingana na seneta huyo wasanii wa mziki hawafai kutegemea kitega uchumi kimoja badala yake wanafaa kupanua vitega uchumi ili kunufaika zaidi.

Bob Mwayele alikuwa msanii wa mziki wa kitamaduni. Alifariki akiwa na umri wa miaka 46.

Taarifa na Dominick Mwambui.

 

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.