Serikali kuchunguza chazo cha mimba za mapema

November 5, 2018

Waziri wa elimu nchini balozi Amina Mohammed amesema kuwa wizara yake imeteua jopo maalum kuchunguza chanzo halisi cha ongezeko la visa vya watahiniwa wa mtihani wa kitaifa wa darasa la nane KCPE kufanya mtihani wakiwa wajawazito.

Akizungumza mjini Mombasa katika afisi za Mshirikishi mkuu wa Utawala Pwani  alipoongoza ufunguzi wa kasha la mtihani wa kidato cha nne KCSE, balozi Amina ameeleza kusikitishwa na ongezeko la visa hivyo mwaka huu.

Kauli ya Bi Amina inajiri baada ya baadhi ya watahiniwa wa mtihani wa darasa la nane hususan kutoka kaunti ya Kilifi  kufanya mtihani wakiwa wajawazito na wengine wakijifungua wakati wa mtihani.

Wakati uo huo waziri huyo wa elimu amesema kuwa wizara yake imejiandaa vyema kuhakikisha kuwa hakuna visa vyoyote vya udanganyifu vitakavyoripotiwa kwenye mtihani wa KCSE ulioanza rasmi mapema leo akiwaonya wenye njama ya kuiba mitihani kuwa watakabiliwa.

Taarifa na Cyrus Ngonyo.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.