Serikali kukarabati madarasa duni asema Kingi

May 11, 2018

Mbunge wa Magarini Michael Kingi amesema serikali imeweka mipango maalum ya kuhakikisha inatatua swala la uhaba wa walimu na ujenzi duni wa madarasa katika shule za eneo bunge hilo.

Michael, amesema tayari amefanya mazungumzo na wadau husika katika sekta ya elimu ili kuhakikisha swala hilo linaafikiwa na wanafunzi wanasoma katika mazingira bora kinyume na inavyoshuhudiwa kwa sasa.
Mbunge huyo wa Magarini amesema taasisi ya mafunzo ya Uwalimu ya Galana Teachers Training College itasajiliwa rasmi katika Wizara ya Elimu ifikapo mwezi Septemba mwaka huu.

Wakati uop huo amehoji kuwa hazina ya ustawi wa maeneo bunge CDF katika eneo hilo imetenga jumla ya shilingi milioni tano za ujenzi wa vyumba vya kulala kwa wanafunzi watakaokuwa shuleni humo.

Taarifa na Esther Mwagandi.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.