Serikali yahimizwa kutolegeza Kamba dhidi ya wafisadi

May 30, 2018

Mashirika ya kijamii nchini yametoa mwito kwa serikali kuhakikisha kuwa wanatuhumiwa wa sakata ya ufisadi ya Huduma ya vijana kwa taifa NYS wameshtakiwa na kufungwa.

Akizungumza na wanahabari mjini Mombasa mshirikishi wa kitaifa wa mashirika ya kijamii Suba Churchil ameihimiza serikali kuendelea kuzifunga akaunti za benki za washukiwa hao ili wasitumie fedha hizo kulipa dhamana na kusalia huru.

Churchil ambaye pia ni msimamizi wa shirika la Civil Society Reference Group amehimiza fedha hizo kuregeshwa katika mfuko wa serikali ili zimfae mwananchi kimaendeleo.

Mashirika hayo yameelezwa kughadhabishwa na jinsi kesi za ufisadi zinavyoendeshwa humu nchini wakiahidi kufuatilia sakata ya sasa hadi washukiwa watakapohukumiwa na kufungwa jela.

Taarifa na Marrieta Anzazi.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.