SERIKALI YAJIPANGA KUMALIZA VISA VYA DHULMA ZA KIJINSIA MAGARINI

December 6, 2017

Serikali ikishirikiana na wadau mbali mbali huko Garashi eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi imesema kuwa imeweka mikakati thabiti ya kumaliza visa vya dhulma za kijinsia dhidi ya watoto wadogo.

Kwa mujibu wa chifu wa eneo hilo la Garashi Ndundi Chula, hatua hiyo imejiri kufuatia ongezeko la watoto kudhulumiwa kimapenzi na wengine wakionekana kuachama masomo.

Chula  amedokeza kuwa dhulma hizo pia zimepelekea idadi kubwa ya watoto kutungwa mimba za mapema hali anayosema imechangia ongezeko la viwango vya umaskini

Taarifa na Esther Mwagandi

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.