Serikali yaombwa kuwashika mkono walioasi Al- Shabaab

December 2, 2017

Mkurugenzi mkuu wa shirika la kijamii la KECOSCE Phyllis Muema ameiomba serikali kuwasaidia vijana walioasi makundi ya kigaidi nchini somalia.

Bi muema amesema kuwa ni vyema iwapo serikali itaweka mikakati ya kuwapa ushauri vijana hao waliotoroka nchini Somalia na kubadili fikra zao baadaye.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa mradi wa ‘Tusemezane Vijana’ unaolenga kutoa mafunzo maalum kwa kamati mbalimbali za vijana katika kila Kaunti, Bi Muema amesema kwamba mradi huo unawahusisha vijana moja kwa moja kwani ndio walengwa wakuu katika swala zima la ugaidi.

Tayari shughuli ya kubuni kamati mbalimbali za vijana mashinani kote Pwani na katika Kaunti ya Garissa inaendelea kabla utoaji mafunzo na ushauri nasaha kwa Vijana kuhusiana na swala la ugaidi na itikadi kali kung’oa nanga mapema mwakani.

Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.