Serikali yaweka mikakati ya kuboresha kiwango cha samaki

November 22, 2017

Serikali ya kitaifa inaendeleza mikakati kuboresha kiwango cha samaki nchini na kuboresha uchumi kupitia sekta ya uvuvi.

Kwa mujibu wa waziri wa Kilimo, uvuvi na ufugaji Willy Bett, serikali inapania kukuza samaki kuimarisha kiwango cha samaki anachosema kiko chini licha ya kuwepokwa raslimali kuu ya bahari.

Waziri Bett amesema kwamba serikali itaidhinisha mikakati kuboresha shughuli za uvuvi nchini ikiwemo kukabiliana na wavuvi wa mataifa ya nje wanaovua humu nchini kinyume cha sheria.

Kwa upande wao wavuvi kutoka eneo la Shimoni wakiongozwa na Omar Mtengo wameitaka serikali kuboresha shughuli za uvuvi kupitia kuwanunulia vifaa bora na vya kisasa kuwawezesha kuvua hadi maji makuu na kupata samaki wengi zaidi.

Taarifa na Mwanakombo Juma.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.