Shambulio la kigaidi Lamu la angamiza watu watatu

August 3, 2017

Imebainika wazi kuwa ni watu watatu waliofariki baada ya kushambuliwa na wanamgambo wa Al-shabab huku wanafunzi wanne wakipata majeraha ya risasi.

Shambulizi hilo  lilitokea jana mwendo wa saa tisa alasiri eneo la Nyongoro huko Witu kaunti ya Lamu kwenye barabara kuu ya Garsen- Lamu.

Akiongea na Wanahabari katika hospitali ya Malindi, Afisa mkuu msimamizi wa hospitali hiyo Hossan Ajuk amesema kuwa wanafunzi hao ni wawili wa kike na wawili wa kiume ambao walikua ndani ya gari la polisi na walikua wakielekea Witu kwa likizo.

Ajuk amesema kuwa kati ya watu watatu waliofariki na kuteketezwa kiasi cha kutotambulika walikuwa maafisa wakuu katika kaunti ya Tana River. Hata hivyo amedokeza kuwa wanafunzi hao wanaendelea kupokea matibabu licha ya mgomo wa wauguzi unaoendelea.

Taarifa hii imeandikwa na Charo Banda.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.