Shehena ya kwanza kubebwa na SGR kutoka Nairobi kuwasili mjini Mombasa

January 8, 2018

Gari moshi la kisasa la kubeba mizigo lililobeba makasha 52 kutoka Jijini Nairobi alfajiri ya leo linatarajiwa kuwasili kwenye kituo kikuu cha Reli mjini Mombasa.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari Mkurugenzi mkuu wa shirika la reli nchini,  mhandisi Athanas Maina amesema kuwa  makasha hayo yaliobeba Majani Chai, Magunia ya Maharagwe aina ya French Beans yatasafirishwa hadi bandarini Mombasa.

Maina amesema kuwa shirika la reli nchini limeidhinisha mikakati ya kuwashirikisha wadau wote wa sekta za kibiashara nchini ili kufanikisha usafirishaji wa mizigo kupitia reli ya kisasa.

Mhandisi Maina amesema shirika la reli nchini limeidhinisha mikakati thabiti kusafirisha mizigo kupitia reli ili kupunguza msongamano wa magari katika barabara kuu nchini.

Taarifa na Cyrus Ngonyo.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.