Sherehe za usiku zapigwa marufuku Kwale

November 8, 2018

Karuku Ngumo Kwale County commissioner

Sherehe za harusi za usiku katika kaunti ya Kwale zimepigwa marufuku.

Kamishna wa kaunti hiyo Karuku Ngumo  ametoa onyo kwa wakaazi wa kukoma kuandaa sherehe za usiku akisema kuwa zinasheheni maovu.

Ngumo amezitaja sherehe hizo ikiwemo harusi na Disco matanga kama chanzo kikuu cha ukosefu wa usalama na zinazopelekea vijana kuporomoka  kimaadili.

Ngumo amewahimiza machifu kuwa chonjo kuhakikisha sheria hio inatekelezwa kama njia mojawapo ya kuboresha usalama hususan nyakati za usiku.

Sikiliza hapa.

MARUFUKU YA HARUSI KWALE

Taarifa na Salim Mwakazi.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.