SHIRIKA LA HURIA LATAKA VITA DHIIDI YA ITIKADI POTOFU KUENDELEZWA

October 26, 2018

Shirika la kutetea haki za kibinadama la HURIA linataka mikakati ya kukabiliana na tatizo la visa vya ugaidi na itikadi potofu miongoni mwa vijana  pwani  kuendelezwa, licha ya visa hivi kupungua.

Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Yusuf Lule Mwatsefu, ameitaka idara ya usalama, ikishirikiana na watetezi wa haki za kibinadamu na idara zengine husika, kujadili mikakati itakayomaliza swala la ugaidi na itikadi potofu hapa pwani.

Lule amesema kwamba juhudi zaidi zinahitajika, kwani magaidi wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali katika kuwahadaa vijana kujiunga na  mitandao hiyo.

Shirika la HURIA tayari linaendeleza vikao katika kaunti za Kwale, Mombasa na Kilifi kujadili mbinu za kumaliza tatizo hili la kiusalama.

Taarifa na Gabriel  Mwaganjoni

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.