Siasa ni sumu michezoni asema mshirikishi wa Samba Sports Youth Agenda

June 21, 2018

Mshirikishi wa shirika lisilo la kiserikali la Samba Sports Youth Agenda, Mohamed Mwachausa, amewatolea wito viongozi wa kisiasa kutoingiza siasa katika maswala ya michezo.

Mwachausa amedai kwamba siasa ni sumu inapoingizwa katika michezo hivyo basi viongozi wanafaa kutenga siasa kando na michezo.

“Siasa na michezo ni vitu viwili tofauti sana. Tunapoingiza siasa kwenye michezo tutakuwa tunauwa ndoto za watu wengi walio na talanta za micheni.”

“Siasa siku nyingi ni mhezo mchafu wa kuchafuliana majina na ahadi za uongo ndiposa hazifai kuingizwa kwenye michezo,” amesema Mwachausa.

Mwachausa aidha amewatolea wito vijana kuanza kuchukua nafasi zao katika jamii kwa kujitolea kwa hali na mali kuona kwamba talanta zao zinakuzwa na kuwasaidia maishani.

“Kila kijana anafaa kujua kwamba talanta yake inauwezo wa kumuokoa maishani iwapo. Ni wito wangu kwa vijana kusimama kidete na kuona kwamba wamejituma kuona kwamba talanta zao zinakuzwa,” amesema Mwachausa.

Vilevile amewahimiza vijana kujeza titin a kuepukana na utumizi wa mihadarati ambao umeathiri zaidi ya vijana elfu tano katika kaunti ya Kwale.

Kwa sasa shirika hilo lisilokuwa la kiserikali lina andaa michuano ya soka ya watoto wasiozidi umri wa miaka 13. Mchuano huo utafanyika wikendi hii mjini Ukunda kaunti ya Kwale.

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.