Sijutii kuosha magari Mama Ngina- Dogo Richie

July 7, 2018

Msanii Dogo Richie anayetamba kwa vibao Fire na Go gaga kwa sasa amesema kuwa hajawahi hata siku moja kujutia kuwa mwoshaji magari katika ufo wa Mama Ngina.

Msanii huyo aliwahi kuwa mmoja kati ya vijana waliopata riziki katika ufuo huo muda mfupi baada yakumaliza shule ya upili.

“Nilikuwa nimekuja mjini kutafuta maisha lakini yule niliyekuja kwake hakuwepo ilinibidi nianze kujitafutia riziki kwa kila njia na kuosha magari ilikuwa mojawapo,” amesema Dogo Richie.

Kupitia uoshaji magari Richie amesema kuwa lipata mtaji wake wa kwanza wa kurekodia wimbo. Wimbo huo ulikuwa na maadhui ya kuwaasia vijana kuhusu virusi vya HIV vinavyosababisha UKIMWI.

“Pale nimefika wale walio na talanta na wanaoweza kujituma pia wanaweza kufika. Maisha ni vile utakavyo yawe, ukiwa mvuvi ole wako ukiwa na bidi utafanikiwa,” amemalizia Dogo Richie.

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.