Simba wamla Papa

June 4, 2018

Timu ya Simba kutoka Tanzania imekanyaga kanyaga papa wa Kariobangi na kufuzu  kwa nusu fainali ya kuwania taji la Sport Pesa Cup kwa ushindi wa 3-2.

Wachezaji wa Kariobangi sharks walishindwa n aukali wa Simba kupitia mikwaju ya penanti. Wachezaji wa Kariobangi Sharks waliocheka na wavu ni Kepkirui na  Harrison Mwendwa, huku  Shiveka Geofrey akidakiwa naye  Erick Juma akitemewa, Michael Bodo alipiga nje.

Wachezaji wa Simba waliofunga ni Niyo Nzima, Erasto Nyonii, Mkude Jonas. Waliopoteza ni Hussein Mohammed, Bukaba Paul. Simba baada ya kumla papa sasa wanalenga kuwala Kakamega Homeboyz siku ya alhamisi.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.