Sofapaka walazimisha sare na Bandari

September 27, 2018

Mkufunzi wa Bandari Bernard Mwalala amesema kuwa alama moja waliyoipata dhidi ya Sofapaka ugani Mbaraki imekuwa na umuhimu mkubwa katika kufanikisha azma yao ya kumaliza katika nafasi ya pili kwenye ligi kuu nchini KPL.

Akizungumza baada ya mechi hiyo Mwalala amesema kuwa japo walilenga kupata alama tatu, sare hiyo imewasaidia kupanua mwanya mkubwa wa pointi 8 zaidi dhidi ya mahasimu wao Sofapaka na Afc Leopards walikokuwa pia wanang’angania nafasi ya pili.

Kwa upande wake mkufunzu wa Sofapaka John Baraza amelalamikia hali duni ya uwanja akisema kuwa imechangia kupatikana sare hiyo.

Kufuatia sare hiyo Bandari inashikilia nafasi ya pili ikiwa na alama 59 alama nane mbele ya sofapaka na leopards wanaoshikilia nafasi ya tatu wakiwa na alama 51 kila mmoja.

Taarifa na Cyrus Ngonyo.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.