SS Assad yataka mechi dhidi ya Gor Mahia ihamishwe

May 24, 2018

ASSAD 2

Meneja wa timu ya SS Assad kutoka ukunda kaunti ya Kwale, Hamisi Dele ameitaka mechi yake dhidi ya Gor Mahia ihamishwe kutoka uga wa Mbaraki hadi uwanja wa maonyesho wa Ukunda.

Dele ameiandikia FKF akisema kuwa uwanja wa Ukunda ndio uwanja wao wa nyumbani na wangependa mashabiki wa nyumbani watizame mechi hiyo kwa wingi.

Assad kwa sasa wako katika nambari tano kwenye jedwali la timu 14 katika ligi ya Division One League Zone A.

Assad wanashiriki mchuano wa Sportpesa Community shield kwa mara ya tatu.

Taarifa na Dominick Mwambui.

 

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.