Stella Mbeyu kusisimua ulingo wa mziki wa Bango

May 10, 2018

Ulingo wa mziki wa Bango unatarajiwa kuwa na msisimuko mpya hivi karibuni baada ya msanii Stella Mbeyu kuweka wazi kuwa analenga kujibu tunzi za wasanii wa kiume wa Bango.

Katika siku za hivi karibuni wasanii wakiume wamekuwa wakitunga mashairi ambayo kwa njia moja au nyingine yameelekezewa wanawake lakini hakujakuwa na jibu kutoka kwa upande huo.

Ni kutokana na hili ambapo Stella Mbeyu ameamua kuchukua jukumu la kuzijibu tunzi hizo.

Baadhi ya Tunzi zitakazo pata jibu ni ile ya Emmanuel Mwamutsi “Mwambire Babayo ahunguze Mali” ya Sunday Ngala na Manu Bayaz “Sio Leo” na vilevile tunzi za Fadhili Bavyombo.

“Ni mchezo tu wakiutunzi wala sina kinyongo na mtu. Naheshimu kazi zao lakini wakati umefika sauti ya wanawake isikike,” amesema Stella Mbeyu.

Taarifa na Dominick Mwambui.

 

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.