Sukari tani 400 zaharibiwa Mombasa

May 12, 2018

Zaidi ya magunia elfu 8 ya sukuri yanayokisiwa kuingizwa humu nchini kimagendo yameharibiwa katika bandari ya Mombasa.

Akiongoza hafla hiyo Waziri wa viwanda nchini Aden Mohammed amesema kuwa sukari hiyo yenye uzani wa tani  400 ilingizwa kinyume cha sheria kutoka nchini Brazil kupitia jina la kampuni moja ya Uganda   ikiwa kwenye makasha 16.

Aden hata hivyo amesema wizara ya uchukuzi nchini haitaruhusu visa hivyo kundelezwa, akisema kuwa hatua hiyo ni kunyima taifa hili ushuru na kudidimiza uchumi.

Kwa upande wake waziri wa utalii nchini Najib Balala amesema kuharibiwa kwa sukari hiyo ni njia moja wapo ya kuimarisha viwango vya biashara humu nchini.

Taarifa na Hussein Mdune.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.