Susumila amwaga razi

December 7, 2018

Msanii Yusuf Kombo maarufu Susumila amemwaga razi kwa watu wanaomkashifu kwa kukubali kushiriki katika show ya Wasafi jijini Mombasa.


Kwenye show hiyo Susumila amepwangwa miongoni mwa kikosi cha wasanii wa Kenya wanaodaiwa kuanza show kabla ya kikosi cha Wasafi. Wanomkashifu msanii huyo wanasema amejishuhsa hadhi. Kupitia kwa ukurasa wake wa Facebook Susumila amesema:

“Jamani show sijaipanga mimi wenye kupanga kimtazamo wao wameona nawafaa kwenye hio show so kama waona sifai panga show yako alafu usiniweke muweke unaempenda ama unaemuona anakufaa mbona tunasahau huwezi pendwa na kila mtu na huwezi chukiwa na kila mtu 😂😂🤣kwa sasa nivumilieni kidogo mpaka 26th ikiisha maisha yataendelea ama mnasemaje wangwana#Mchezousiuchezee.”

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.