Tapeli wa mtandaoni asakwa Mtwapa

October 7, 2018

Maafisa wa ujasusi katika eneo la Pwani wanamuandama mshukiwa mmoja wa uhalifu kupitia utandawazi aliyewatapeli wasimamizi wa hoteli ya kitamaduni ya Afrika Kenya Village-Kijiji eneo la Mtwapa Kauti ya Kilifi.

Kulingana na Meneja wa hoteli hiyo ya kitamaduni Maxwell Chogo, tapeli huyo kwa jina la Andrea Baraka amekuwa akiwaleta wageni katika hoteli hiyo na kisha kutoweka na fedha baada ya kufungua mtandao sawia na ule wa hoteli hiyo.

Kwa upnde wake, Afisa anayesimamia maslahi ya wageni hotelini humo George Masika amedhihirisha hofu yake kutokana na utapeli huo katika sekta ya utalii Pwani.

Masika hata hivyo amewasihi wageni wa hapa nyumbani na wale wa kigeni kamwe kutohofia kuzuru hoteli hiyo ya kitamaduni licha ya tukio hilo la utapeli akiwahakikishia kwamba tayari Baraka anaandamwa na Maafisa wa Idara ya upelelezi.

Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.